Loading...
title : DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA
link : DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA
DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro jana Ijumaa Novemba 3,2017 amewatembelea wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kuwahamasisha kulima zao hilo kwa njia za kitaalamu/kisasa ili kilimo hicho kiwe na tija kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.
Akizungumza katika kikao na wananchi wa kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo cha pamba,Matiro aliyekuwa ameambatana na wataalamu wa zao la pamba,aliwataka wakulima wa zao hilo wilayani humo kulima kisasa kwa kufuata kanuni 10 za kilimo ikiwemo kulima kwa kutumia kamba.
Alisema wananchi katika wilaya hiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kulima zao la pamba lakini wamekuwa hawapati faida kutokana na kulima njia zisizo za kitaalamu.
“Tunataka kufanya kilimo biashara ili kiwe na tija,hatupati mazao ya kutosha kutokana na kutolima kitaalamu,naomba mwaka huu tuwasikilize wataalamu wetu wanatuambia nini,nataka tubadilishe maisha yetu kupitia pamba”,alisema Matiro
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza leo akiwahamasisha kufuata njia za kisasa kulima zao la pamba-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza wananchi kulima mazao ya biashara pamoja na yale ya chakula
Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza katika kikao hicho
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akitoa elimu kwa wakulima wa pamba juu ya njia ya kisasa ya kulima zao hilo
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akionesha kamba zinazotakiwa kutumika katika kilimo cha pamba.
Hivyo makala DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA
yaani makala yote DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dc-shinyanga-akutana-na-wakulima-wa.html
0 Response to "DC SHINYANGA AKUTANA NA WAKULIMA WA PAMBA SHINYANGA VIJIJINI KUHAMASISHA KILIMO CHA KISASA"
Post a Comment