Loading...
title : DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO
link : DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO
DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO
Taasisi ya Dr Mtuyabaliwe imekabidhi Chumba cha maktaba, ilichokikarabati na kukisheheni vitabu, kwa shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke, ambayo tangu kuanzishwa kwake miaka 30 iliyopita haikuwahi kuwa na maktaba.
Akikabidhi Maktaba hiyo Mkurugenzi na Muasisi wa Taasisi ya Dr Ntuyabakiwe Jacquiline Mengi amesema Taasisi hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2015 kumuenzi marehemu baba yake aliyekuwa mpenzi mkubwa wa kusoma vitabu, inahimiza usomaji wa vitabu kwa wanafunzi,ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali za kutoa elimu bora nchini:
Katika salaamu zao za shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Bakari Makele, Mwalimu Mkuu Esther Matowo na Dada mkuu Veronika Mruma wameshukuru kwa msaada huo na kuahidi kuitunza na kuitumia ipasavyo.
Wakati wa hafla hiyo Mwakilishi Taasisi ya Sema-Tanzania Itanisa Mbise alikabidhi kwa Dada Mkuu wa shule Veronica Mruma nakala 100 za jarida linalochapishwa na Taasisi hiyo kwa matumizi ya maktaba hiyo.
Makabidhiano ya Makataba hiyo kwa shule ya Msingi Muungano yamefanyika wakati ambao Wizara ya elimu imeingiza somo la Maktaba katika mtaala wa elimu baada ya kuona umuhimu wake katika kufanikisha utoaji wa elimu katika shule za msingi.
Dr Ntuyabaliwe Foundation ni taasisi pekee binafsi nchini inayojihusisha na utoaji wa misaada ya vitabu vya maktaba kwa shule za msingi nchini, na hadi sasa imekwishatoa misaada kama huo kwa shule mbili za msingi za jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muungano waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akikata utepe kuashiria uzikizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo katika shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke
Mwalimu Mkuu ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo akisoma risala kwa mgeni rasmiwakati wa zoezi la uzinduzi wa maktaba shuleni hapo leo. wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke, Bakari Makele.

Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO
yaani makala yote DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dr-ntuyabaliwe-foundation-yakabidhi.html
0 Response to "DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO"
Post a Comment