Loading...
title : EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC
link : EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC
EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC
KADRI siku zinavyokwenda mbele, wadau wanaoguswa na sanaa hapa nchini wanasaka namna ya kusaidia tasnia hiyo ambayo ni eneo adhimu kwa jamii duniani. Mara nyingi wasanii wamekuwa wakilalamika kwamba wanafanywa kama yatima ambao wanakosa msaada wa kuwasogeza katika njia ya maendeleo baada ya kufanya kazi zao kwa ufanisi. Wasanii hulalamika katika matukio mbalimbali ya kazi zao, hali ambayo husababisha kuonekana kwamba tasnia hiyo sio eneo la kukimbilia kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii.
Wasomi wa Sanaa hapa nchini wanaguswa kwa kiasi kikubwa na sanaa za Tanzania ambao wanatekeleza kwa vitendo kazi hizo, Asasi ya East Africa Art Biennale (EASTAFAB) inaguswa na malalamiko, vilio vinavyotolewa na baadhi ya wasanii katika matukio yanayoandaliwa na baadhi ya wadau wanaoguswa na mdororo wa maendeleo ya kazi za sanaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa EASTAFAB, Dr. Kiagho Kilonzo anasema mguso huo umejikita kwenye kupromoti sanaa za Ufundi ambazo zina idadi kubwa ya wasanii ambao wakiwemo Wachongaji, Wachoraji, Wasusi, Wafinyanzi na wengineo ambao wanaingia kwenye Sanaa za Ufundi.
Dr. Kilonzo anasema promosheni hiyo hufanyika kupitia Maonesho ya Sanaa ambayo yalianza tangu mwaka 2003 ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili. Anasema mara zote 7, maonesho hayo ya Afrika Mashariki yamekua yakifanyika jijini Dar es Salaam ambayo pia hushirikisha wasanii wengine kutoka nje ya Afrika Mashariki na kushirikisha wasanii wa Afrika, Ulaya na Amerika lakini mwaka huu limepanua wigo kwa kufanyika katika majiji ya Afrika Mashariki.
Anasema pamoja na kufanyika katika majiji ya Afrika Mashariki pia kutakuwa na semina ya wasanii na matukio mengi yanayoendana na mwenendo wa hali ya sanaa pamoja na masoko ya sanaa.Dr. Kilonzo anasema katika semina hiyo itakayofanyika Novemba 3, kutakuwa na wawasilishaji mada wa nchi za Tanzania (kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania), Revocatus Kundy, Kenya (kutoka Taasisi ya Elimu Kenya), Dr. Jennifer Wambugu na Uganda (kutoka Kituo cha Maendeleo ya Mitaala), Christopher Muganga.
Katika semina hiyo mbali ya watoa mada kuchanganua mipangilio mbalimbali ya sanaa pia wasanii watajadili hoja mbalimbali zitakazowasilishwa mezani na watoa mada. Dr. Kilonzo anasema pamoja nao katika semina hiyo kutakuwa na wahusika wa masoko ya sanaa hapa nchini ambao ni pamoja na Origenes Uiso (Karibu Art Gallery), Abel Shuma (Alliance Francaise), Tim Amstrong kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Franciscar Shirima-Frankoo Design.
Anasema semina hiyo itafanyika nyumbani kwa Balozi wa Uswiss, Arthur Mattli Masaki mtaa wa Kenyata Drive jijini Dar es Salaam ambaye pia atazindua maonesho hayo Novemba 4 katika kituo cha Nafasi Art Mikocheni jijini Dar es Salaam huku ufunguzi wa kwanza utafanyika Novemba 2 ambao utafanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Olle Gabriel.
Dk. Kilonzo anasema mgeni rasmi Novemba 3 atakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu, Habib Fent.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC
yaani makala yote EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/eastafab-kibwebwe-kinachopigia-chapuo.html
0 Response to "EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC"
Post a Comment