Loading...
title : KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO
link : KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO
KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO
LIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO
Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake mara baada ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa wachezaji watatu kwa kila timu.
Awali, CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji kwa mwaka huu kuwa 23.
Wachezaji walioongezwa na Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Young Africans ya Dar es Salaam, Amani Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
Kikosi cha wachezaji 20 wa awali wa Ninje - Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).
Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans).
Washambuliaji ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman), Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).
Benchi la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Hivyo makala KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO
yaani makala yote KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/kilimanjaro-stars-yaongeza-watatu.html
0 Response to "KILIMANJARO STARS YAONGEZA WATATU, KULIFUATA KOMBE LA CHALENJI KESHO"
Post a Comment