Loading...
title : King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja
link : King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja
King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja
Kocha wa Miembeni City, Mohammed Seif "King"
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kocha Mkuu wa timu ya Miembeni City Mohammed Seif "King" amekiri hali ya klabu yake si nzuri kufuatia kucheza michezo saba mfululizo bila ya kupata ushindi hata mchezo mmoja katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja.
King amesema kwa mara ya kwanza anakumbana na matokeo mabaya katika maisha yake ya soka lakini bado hajakata tamaa kwenye ligi hiyo huku akiamini vijana wake watapambana kufa na kupona ili wabakie kwenye ligi Kuu.
"Balaa balaa, katika historia yangu kwa mara ya kwanza nakumbana na matokeo mabovu kama haya, nakiri tuna matatizo lakini tutapigana kufa kupona ili tubakie kwenye ligi, na kushuka daraja pia sio dhambi lakini vijana watahakikisha tunabakia". Alisema King.
Miembeni City ipo nafasi ya 13 wakiwa na alama 1 tu kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja kufuatia kufungwa michezo 6 na kwenda sare mchezo mmoja ambapo mpaka sasa City wapo kwenye mstari mwekundu kwenye ligi hiyo yenye jumla ya timu 14 ambapo timu 6 za chini zitalazimika kushuka daraja.
Hivyo makala King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja
yaani makala yote King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/king-akiri-hali-ya-miembeni-city-ni.html
0 Response to "King akiri hali ya Miembeni City ni ngumu, ahakikisha kutoshuka daraja"
Post a Comment