Loading...
title : KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI
link : KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI
KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa muda wa siku 21 kwa Mkandarasi Nyanza Road Works kuongeza vifaa vya kazi na wafanyakazi ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Mhe. Kwandikwa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma leo, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa ujenzi huo unatakiwa kukamilika haraka ili kuweza kufungua mkoa huo na kurahisha shughuli za usafirishaji.
“Hakikisheni ndani ya wiki tatu vifaa vya ujenzi vinakuwepo eneo la kazi na ajira zinatolewa kwa wananchi ili mradi ukamilike mapema iwezekanavyo”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.Kuhusu suala la malipo, Mhe. Kwandikwa amefafanua kuwa hivi sasa hakuna tatizo lolote la malipo kwani mkandarasi ameshalipwa na kilichobaki sasa ni mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili ujenzi ukamilike.
“Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi anazozifanya kwani hivi sasa hali ya fedha ni nzuri, mapato yanaongezeka hivyo tutegemee kupata matunda ya maendeleo ya miundombinu bora hapa nchini”, amesema Naibu Waziri Mhe. Kwandikwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), akikagua kalvati katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (aliyevaa suti) akikagua matofali katika kambi ya mkandarasi ya Nyanza Road Works alipokuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inaojengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura (kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), aina ya kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Hivyo makala KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI
yaani makala yote KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/kwandikwa-atema-cheche-kwa-mkandarasi.html
0 Response to "KWANDIKWA: ATEMA CHECHE KWA MKANDARASI KUONGEZA MITAMBO NA WAFANYAKAZI"
Post a Comment