Loading...

Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo

Loading...
Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo
link : Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo

soma pia


Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amempa maelekezo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuunda Kamati ya kuchunguza uvamizi wa viwanja vya Gereza Isanga uliofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi katika Gereza hilo, Masauni alisema eneo hilo ambalo lina ukubwa wa ekari zaidi ya 150 lazima lirudishwe katika himaya ya Jeshi la Magereza kama lilivyokua awali. “Eneo hili linalimilikiwa na Jeshi la Magereza tangu mwaka 1946, haiwezekani watu watokee na kuchukua ardhi hii kiholelaholela, hii haiwezekani hata kidogo, lazima uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo na eneo lote lilrudi mikononi mwa jeshi,” alisema Masauni na kufafanua;

“Serikali ilishahamia hapa mjini Dodoma, hivyo shughuli za magereza zitaongezeka kwa kasi, na umuhimu wa maeneo utakua mkubwa zaidi kutokana na umuhimu wa jeshi hili katika kukuza uchumi.” Aliongeza kuwa, jeshi hilo linahitaji kujenga nyumba za askari kwa kasi na kutokana na changamoto hiyo ya uvamizi uliofanywa ujenzi waweza kusuasua hivyo eneo hilo lahitajika kurudishwa haraka sana.

Masauni alifafanua kuwa, tayari amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali, Projest Rwegasira kulichunguza suala hilo kwa kina kwa kuwa kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kuwa kati ya wamiliki wa viwanja hivyo walikua ni viongozi waandamizi wa CDA, Jeshi la Magereza pamoja na viongozi wakubwa mbalimbali.

Hata hivyo, Masauni alipiga marufuku mtu yeyote kuendeleza ujenzi wa eneo hilo hata kama ana vibali vyote vya kumiliki eneo. Aidha, Mkuu wa Gereza Isanga, Keneth Mwambeje, akizungumzia suala hilo, alisema jeshi lake lina nyaraka za mawasiliano kati ya viongozi wa gereza hilo ambao walikua kwa wakati huo pamoja na wa CDA.

CDA ambayo ilivunjwa na Rais John Magufuli, ndio inahusika kugawa viwanja hivyo kwa wananchi zaidi ya mia moja ambao baadhi yao wamejenga na wengine wanaendelea na ujenzi katika eneo.


Hivyo makala Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo

yaani makala yote Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/masauni-aitunishia-misuli-cda-uvamizi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Masauni aitunishia misuli CDA uvamizi wa viwanja Magereza Dodoma, apiga marufuku wananchi kuendeleza ujenzi eneo hilo"

Post a Comment

Loading...