Loading...
title : Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti
link : Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti
Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3 kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la kuombea fedha kwa ajili ya tafiti. Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam.
Akizungumza Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa.
Alisema kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda nchini. “Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi Alisisitiza umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda.
Aliongeza kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Alisisitiza kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini. Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti.
Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia program ya TTI , Julie LaFrance, amesema kwamba ni muhimu kwa watafiti kuendelea na utafiti endelevu na wa kina ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii ya watu baada ya kupata matokeo baada ya utafiti.
Aliongeza kwamba baada ya semina hiyo watafiti wa ndani watakuwa wamepata uelewa mkubwa wa kuandika mapendeko thabiti na bora zaidi yenye kuvutia wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kuanza kuwapa fedha kwa ajili ya tafiti zenye tija nchini. Warsha hiyo pia iliwakutanisha watafiti kutoka Taasisi ya IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na chuo cha Jamii kutoka Ghana.
Hivyo makala Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti
yaani makala yote Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/matukio-esrf-yawezesha-warsha-ya-andiko.html
0 Response to "Matukio : ESRF Yawezesha Warsha ya Andiko Thabiti la Thabiti"
Post a Comment