Loading...
title : MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA.
link : MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA.
MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde leo amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 60 mshindi wa droo ya Tatumzuka Bwana Robert Changadiko ambaye alijishindia kiasi hicho katika ‘Jackpot’ ya wiki hii katika droo ya kusisimua iliyoonyeshwa siku ya jumapili kupitia vituo vya runinga kote nchini.
Bwana Changadiko ambaye anafanya kazi kama fundi minara mjini Dodoma alielezea furaha yake juu ya ushindi huo ambao hakuutegemea na akaishukuru Tatumzuka kwa kutimiza hitaji lake la pesa wakati alipokuwa akizihitaji zaidi.
"Niliamua kucheza Tatu Mzuka kutokana na matatizo niliyokuwa nayo ya kifedha ambapo nilihitaji fedha za haraka ili kukidhi mahitaji hayo. Kwakweli nina furaha kubwa sana na nashukuru kwamba nilijaribu bahati na ikatimia” alisema.Mavunde alimpongeza mshindi kwa kushinda kiasi hicho na Tatu Mzuka kwa ajili ya kuendelea kutengeneza mamilionea na kubadilisha maisha ya watu.
Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira (kushoto) Mh. Antony Mavunde (Mbunge), akimkabidhi mshindi wa 14 wa mchezo wa tatu Mzuka Bw. Robert A. Changadiko(45), hundi ya shilingi milioni sitini , Mjini Dodoma.
Mshindi wa droo ya 14 ya Tatu Mzuka Bw.Robert A. Changadiko (kulia)aliyejishindia donge nono la shilingi milioni sitini wiki hii, akiwa na rafiki yake bwana Bw. Daudi Mwangoto (katikati), ambaye alizawadiwa shilingi milioni moja kutoka katika promosheni ya cheza na washkaji shinda na washkaji ya Tatu Mzuka, kushoto ni Bw.Edwin Kawito ni mshindi wa Tatu Mzuka droo ya kumi (10) aliyejishindia shilingi milioni sitini.
Mshindi wa shilingi milioni sitini kutoka kijiji cha Msembata (Dodoma)Bw.Robert A. Changadiko mwenye umri wa maika 45, ambaye ni fundi minara,akifurahia ushindi wake.
Hivyo makala MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA.
yaani makala yote MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mavunde-amkabidhi-kitita-cha-milioni-60.html
0 Response to "MAVUNDE AMKABIDHI KITITA CHA MILIONI 60 MSHINDI WA DROO YA 14 YA TATUMZUKA MJINI DODOMA."
Post a Comment