Loading...
title : Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa
link : Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa
Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa
Kampuni za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri, mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
“Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015 tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana.
Lakini kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs, "Kimsingi hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood (Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood (Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’.
Kwa sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na kuongeza. "Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au ‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?”
Hivyo makala Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa
yaani makala yote Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mfumo-wa-kutengeneza-na-kusambaza.html
0 Response to "Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa"
Post a Comment