Loading...

MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1

Loading...
MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1
link : MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1

soma pia


MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1



Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Irenius Ruyobya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Oktoba, 2017 ambao umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017. Kulia Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei Bi. Ruth Minja.

Na: Veronica Kazimoto,
Mwambawahabari.
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Irenius Ruyobya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) amesema kupungua kwa Mfumuko wa Bei kunamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Septemba, 2017.

Ruyobya ameongeza kuwa, kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2017 kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba, 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2016.

"Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa Mfumuko wa Bei  ni pamoja na unga wa mtama kwa asilimia 2.6, samaki kwa asilimia 7.1, matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia 7.4, maharage kwa asilimia 2.9, viazi kwa asilimia 14.4 na karanga kwa asilimia 7.8", amesema Ruyobya.

Akizungumzia Mfumuko wa Bei kwa upande wa Afrika Mashariki, Irenius Ruyobya amesema Mfumuko wa Bei wa Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi asilimia 5.72 kutoka asilimia 7.06 mwezi Septemba, 2017 na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.8 mwezi Oktoba, 2017 kutoka asilimia 5.3 mwezi Septemba, 2017.

Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.



Hivyo makala MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1

yaani makala yote MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mfumuko-wa-bei-wapungua-kutoka-asilimia_8.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 5.3 HADI ASILIMIA 5.1"

Post a Comment

Loading...