Loading...

Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet

Loading...
Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet
link : Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet

soma pia


Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet


Mkazi wa Iringa, Alex Kalinga (26) amejishindia kitita cha sh milioni 161 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

Kalinga alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley kwa kushirikiana na Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.

Malley alisema kuwa Kalinga alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12.Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 29 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.

“Ni faraja kubwa kuona kijana mwenye umri wa miaka 26 akishinda mamilioni ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja tu, hii imedhihirisha kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kalinga alisema kuwa hakuamini taarifa ya kushinda mchezo huo mara baada ya kupokea simu ya kujulishwa kushinda.

“Nina furaha sana, mimi ni fundi wa kuchomelea mageti ya chuma, sikuwa na kipato kikubwa pale Iringia Mjini, nitaanza kujenga nyumba na kufungua kiwanda cha kuchomelea na nyingine kusaidia familia yangu,” alisema Kalinga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
 Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (katikati) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 161. Kuliakushoto ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 161.


Hivyo makala Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet

yaani makala yote Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mkazi-wa-iringa-ashinda-milioni-161-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkazi wa Iringa ashinda milioni 161 ya M-bet"

Post a Comment

Loading...