Loading...
title : Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart
link : Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart
Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart
kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa.
Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema, 'Kwa niaba ya wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za sanaa Dar es Salaam.
Tuko tayari kushirikiana nawe kila wakati kwa lengo la kuboresha mazingira yanayohusu uboreshwaji wa stahiki za wanamuziki wakati wowote.Tunarudia tena kushukuru kwa hili'
Msama amekuwa akifanya kazi hii ya kukamata kazi zisizo halali kwa miaka mingi, na Kitime amekuwa mwanaharakati wa swala la Hakimiliki kwa miaka mingi pia.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali,Msama Auction Mart Alex Msama akizungumza na Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar,kuhusiana na hatua aliyofikia ya kuwakamata maharamia wa kazi zaWasanii na Wakwepa kodi kupitia tasnia hiyo,ampao pia amewashukuru wadau wa Muziki mbalimbali wakiwemo Mtandao wa Muziki Tanzania kumpongeza na kumuunga mkono katika mapambano hayo ya kazi za Wasanii hapa nchini
Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime
Hivyo makala Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart
yaani makala yote Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mtandao-wa-muziki-tanzania-umempa.html
0 Response to "Mtandao wa Muziki Tanzania umempa hongera Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart"
Post a Comment