Loading...

MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE

Loading...
MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE
link : MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE

soma pia


MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE

Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ametoa msaada wa pampu ya maji na mifuko 10 ya saruji vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji katika kitongoji cha Mwamapalala kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga. 

Mukadam amekabidhi msaada huo wa pampu ya maji na mifuko ya 10 ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu leo Ijumaa Novemba 17,2017 kwa ajili ya mradi wa maji katika mtaa wa Mwamapalala katika kata hiyo ambayo inakabiliwa na kukosekana kwa huduma ya maji. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,Mukadam alisema hivi karibuni alitembelea kata ya Chibe,ndipo diwani wa kata hiyo akaomba msaada wa kutafutiwa pampu ya maji baada ya wananchi kujitolea kuchimba kisima kirefu. 

“Kutokana na ombi hilo,nimetafuta wafadhili na kupata msaada huu kutoka kwa Farana Hirji aliyenipatia fedha kwa niaba ya Roshan Chatur nikanunua pampu hii na saruji hii itakayotumika kukamilisha ujenzi wa kisima”,alieleza Gulam. 

“Kupitia msaada huu wananchi wa Chibe watapata huduma ya maji safi na salama kwani mhandisi wa maji wa manispaa amefika katika kisima hicho na kutuhakikishia kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu”,alisema Mukadam. 
Zoezi la kushusha pampu ya maji kwenye gari likiendelea wakati Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi pampu ya maji na mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu cha maji katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Kaimu Mhandisi wa maji manispaa ya Shinyanga Nkinda Seni (wa nne kushoto) akishusha mabomba ya pampu ya maji.Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa kukabidhi pampu ya maji na mifuko ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu katika mtaa wa Mwamapalala. Kushoto ni pampu ya maji na mifuko ya saruji. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishikana mkono na diwani wa kata ya Chibe John Kisandu wakati wa akikabidhi pampu ya maji na mifuko ya saruji.Wa kwanza kulia ni Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Rajabu Masanche wakishuhudia zoezi la makabidhiano. 



Hivyo makala MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE

yaani makala yote MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mwenyekiti-wa-alat-na-meya-wa-manispaa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE"

Post a Comment

Loading...