Loading...
title : NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM
link : NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM
NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa amefanya ziara katika kivuko cha Kigamboni na kujionea namna mashine mpya za kieletroniki zilivyoweza kufungwa na kumtaka mhandisi aanze kuzifanyia majaribio kabla ya mwaka huu kuisha ili Januari 2018 zianze kutumika.
Akizungumza baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna wafanyakazi wanavyotoa huduma kwa abiria wanaofika kwa ajili ya usafiri kwa kivuko kutoka Kigamboni na Kivukoni, Naibu Waziri Kwandikwa amesema kuwa amefurahishwa na huduma zinazotolewa na zaidi amezungumza na baadhi ya wananchi na wote wameonekana kufurahishwa.
" Nimezungumza sehemu mbalimbali na kujionea namna watoa huduma wanavyotoa huduma zao kwa abiria na pia nimezungumza na takribani wananchi kumi wanaotumia usafiri wa kivuko na wote wameonekena kufurahishwa na huduma zenu ,"alisema Naibu Waziri Kwandikwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na mhudumu wa kukata tiketi katika kituo cha Kivukoni wakati alipofanya ziara kuangalia namna abiria wanavyopata huduma zao, juu akikata tiketi ya kuingia ndani.
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake katika kivuko cha Kivukoni na Kigamboni na kujionea uendeshaji wa huduma bora kwa abiria kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza na Mhandisi wa kivuko Ally Daudi na akipewa maelezo ya maendeleo ya vivuko vyote vilivyopo chini ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikagua mashine za kieletroniki za tiketi zilizofungwa katika Kivuko cha Kigamboni na Kivukoni wakati wa ziara yake iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/naibu-waziri-wa-ujenzi-kwandikwa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA UJENZI KWANDIKWA ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA VIVUKO JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment