Loading...
title : NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden
link : NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden
NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden
Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya. Mchezaji huyo, aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya hukoanatarajiwa kurejea nchini siku ya Jumatatu inayokuja.
Na mara baada ya kurejea klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko. Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi. Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.
Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa.
Imetolewa na.....
HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari na mawasiliano, Simba Sports Club.
Hivyo makala NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden
yaani makala yote NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/news-alert-mchezaji-said-hamis-juma.html
0 Response to "NEWS ALERT: Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) afuzu majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya Sweden"
Post a Comment