Loading...
title : Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama
link : Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama
Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan ameilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juu ya mashahidi kutofika mahakamani licha ya kesi inayomkabili kupangwa kusikilizwa mfululizo na kuuliza iko wapi kauli ya Rais Magufuli ya hapa kazi tu.
Feng anakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi anadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 13 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Katika kesi hiyo anashtakiwa pamoja na watanzania wawili Salvius Matembo na Philemon Manase.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, mshtakiwa Feng amedai kuwa alimsikia Jaji Mkuu akisema kesi zote za zamani zimalizike kwa Haraka, lakini kesi yake imekuwa ikipangiwa kusikilizwa mfululizo mara lakini shahidi anayetakiwa kutoa ushahidi hajawi kwenda mfululizo hata mara moja.
"Magufuli anasema hapa kazi tu, nikasema sasa mahakama ile kazi haipo kwa haraka, nipo mahabusu naumwa moyo, misuli inauma, kidole kimekufa ganzi, lakini najitahidi nakuja". aliomba kesi ikipangwa tarehe nyingine mashahidi waje na kuuliza kama shahidi mmoja anaumwa je wengine wote wanaumwa?
Mshtakiwa Feng amedai hayo baada ya wakili wa serikali, Wankyo Simon kuieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kusikilizwa lakini shahidi aliyetarajiwa kutoa ushahidi anaumwa, hali yake bado siyo nzuri.
Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko, aliomba mahakama iliangalie hilo na kuwa waendelee na mashahidi wengine wa upande wa Mashtaka katika kuokoa muda.
Wakili Wankyo alidai kuwa katika hali ya kawaida ni lazima shahidi huyo amalizie kutoa ushahidi wake. Hakimu Shaidi aliutaka upande wa Mashtaka kupelekwa mashahidi kama huyo hatakuwa hajatengemaa.
Kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa Mfululizo, Novemba 21,24,27,28,29,30 na Decemba Moja.
Hivyo makala Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama
yaani makala yote Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/raia-wa-china-anayedaiwa-kuwa-malkia-wa.html
0 Response to "Raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu ailalamikia Mahakama"
Post a Comment