Loading...
title : RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO
link : RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO
RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amemtembelea na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde ambapo mwenyekiti huyo wa Wazee amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa Wazee wakati wote wa uongozi wake Mkoani Dodoma.
Dkt. Mahenge alimtembelea Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Balozi (Mstaafu) Lusinde kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma na kuahidi kuwa atakutana na Baraza zima la Wazee la Mkoa wa Dodoma hivi karibuni, aidha, Dkt. Mahenge alipata pia fursa ya kumtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kujionea shughuli za kilimo na ufugaji wa kisasa wa mifugo, nyuki na samaki.
Balozi (Mstaafu)Lusinde amebainisha kumfahamu Mheshimiwa Dkt. Mahenge kwa muda mrefu akiwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na kumpongeza kwa jitihada zake za kuongoza na kutumikia wananchi kwenye nafasi mbalimbali alizowahi kutumika hivyo kumuhakikishia ushirikiano kutoka kwa baraza la wazee.
“Wakati wote wa uongozi wako hapa Mkoani Dodoma, Baraza la Wazee litakuunga mkono na kukupatia ushirikiano mkubwa ili uweze kutekeleza majukumu yako hususani ya kusimamia shughuli za maendeleo kwenye Mkoa wa Dodoma” alisisitiza Balozi Lusinde wakati wa mazungumzo yake na Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Dodoma Balozi Mstaafu Job Lusinde alipomtembelea nyumbani kwake Uzunguni Mjini Dodoma, Balozi Lusinde amemuhakikishia Dkt. Mahenge ushirikiano kutoka kwa wazee.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge kwenye mradi wake mpya wa ufugaji samaki wakati Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge wakati Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtembeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge kwenye mradi wake mpya wa ufugaji samaki wakati Dkt. Mahenge alipomtembelea Mhe. Pinda nyumbani kwake Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Hivyo makala RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO
yaani makala yote RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/rc-mpya-dodoma-dkt-mahenge-awatembelea.html
0 Response to "RC MPYA DODOMA DKT. MAHENGE AWATEMBELEA VIONGOZI WA BARAZA LA WAZEE DODOMA, WAMUAAHIDI USHIRIKIANO"
Post a Comment