Loading...

SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

Loading...
SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA
link : SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

soma pia


SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

SERIKALI haijatoa ruhusa kwa Chuo Kikuu Huria (OUT) kiendelee kutoa kozi ya ‘Foundation’ kama ambavyo imedaiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Baadhi ya mitandao ilitoa taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho: Waziri Mkuu aruhusu kozi za 'Foundation' Chuo Kikuu Huria kwa madai kuwa alitoa ruhusa hiyo jana (Alhamisi, Novemba 30, 2017) wakati akiwa mkoani Singida ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu hicho.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Singida waliohudhuria mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki mjini Singida, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanyia maboresho Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014.

“Kwa sasa Serikali inafanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo kwani sera tuliyonayo haifafanui vizuri jinsi ya kuwasaidia vijana wetu wajiendeleze kwa njia ya mfumo wa elimu huria na masafa,” alisema.

“Programu kama zilizoelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo za Foundation, zinahitaji pia kufafanuliwa kwenye sera yetu, ambayo kwa sasa wataalamu wetu wanaendelea kuiboresha. Pindi itakapokamilika, tutaitolea taarifa kwa Chuo Kikuu Huria na wataalamu wataweza kushirikiana na sekta zote ili kuhakikisha jambo hili linakwenda vizuri,” alisema.

Mapema, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Tozo Bisanda alisema wamepokea barua kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwaarifu juu ya nia ya Serikali kutaka kurejeshwa kwa kozi za Foundation katika chuo hicho.

“Tayari tumekwisha wasilisha mtaala wa Foundation ulioboreshwa ili kukidhi matakwa ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na tunasubiri mrejesho kutoka Kamisheni baada ya kikao chao, mapema mwezi ujao,” alisema Prof. Bisanda.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.

IJUMAA, DESEMBA MOSI, 2017    


Hivyo makala SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA

yaani makala yote SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/serikali-haijaruhusu-kozi-za-foundation.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU HURIA"

Post a Comment

Loading...