Loading...

TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE

Loading...
TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE
link : TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE

soma pia


TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE


Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.
Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.
Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapa chini…
Ofisi ya Spika ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.

Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.
Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:
“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”
Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.



Hivyo makala TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE

yaani makala yote TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/taarifa-ya-ofisi-ya-bunge-kuhusu-lazaro.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAARIFA YA OFISI YA BUNGE KUHUSU LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE"

Post a Comment

Loading...