Loading...
title : TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA
link : TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA
TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA
Na Dotto Mwaibale, Urambo Tabora
TAFITI za kilimo zinazofanywa hapa nchini na wataalamu zimewafikia wakulima wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo Adamu Malunkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109 na mihogo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji nane vya Isongwa, Ussoke, Usisya, Kapiluka, Vumilia, Kamalendi, Muungano na Songambele.
Alisema mara nyingi tafiti zilizokuwa zikifanyika zilikuwa zikibaki kwenye makabati bila ya kuwafikia walengwa na jambo lililofanywa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kuwafikishia wakulima matokeo ya tafiti hizo ni jambo zuri na limefurahiwa na kwa hapa kwetu ni mara ya kwanza kutokea.
"Tuna amini kuwa hivi sasa uchumi utastawi kuanzia ngazi ya familia, wilaya na hadi taifa na tutakuwa na chakula cha kutosha" alisema Malunkwi.
Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha uchimbaji wa mashimo kabla ya kupanda mbegu hiyo ya mahindi.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Isongwa, Shabani Rajabu Mkokoteni , akichimba mashimo.
Mtafiti, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga, mkoani Morogoro, akionesha, akionesha namna ya kuweka mbolea kwenye mashimo yaliyochimbwa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika uzinduzi wa mashamba darasa hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi, Phillips Mtiba, akipanda mahindi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA
yaani makala yote TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/tafiti-za-kilimo-zawafikia-wakulima-wa.html
0 Response to "TAFITI ZA KILIMO ZAWAFIKIA WAKULIMA WA WILAYA YA URAMBO KWA MARA YA KWANZA"
Post a Comment