Loading...

Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC

Loading...
Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC
link : Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC

soma pia


Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC


KUTOKANA na ushirikishwaji wa wakulima wadogo katika zao la chai kupitia Kampuni ya Kuhudumia Wakulima Wadogo Njombe (NOSC), viongozi wa Mkoa wa Njombe wanajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha chai kilichosaidia kuinua kipato cha wakulima wadogo na kuongeza fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Njombe, Bwana Lameck Noah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka mkoani hapa jana katika mahafali ya mwaka mmoja kuhusiana na mafunzo ya kilimo cha chai kilichohusisha wakulima zaidi ya 206.

“Katika mkoa wetu tulijiwekea utaratibu kuwa kila mkulima alime mazao ya aina mbili ya chakula na biashara, kwa upande wa chai tatizo lilikuwa ni aina ya miche, ilikua inachukua muda mrefu kukua lakini tunaishukuru NOSC imetuletea mice inayokua kwa miezi 12 mkulima anaanza kupata majani mabichi ya chai,” alisema Bw. Noah.

Alibainisha kuwa elimu hiyo ina maana kubwa kwa mkoa wake kwa sababu itawasaidia kulima kisasa na kuwaongezea kipato wananchi wa mkoa huo, lakini pia viwanda vitapata malighafi hiyo muhimu kwa ajili ya soko la ndani na nje.

“Tunafahamu chai inapendwa na mataifa ya magharibi, zao hili lina fedha nyingi za kigeni. Soko la chai lipo na tunawahakikishia wakulima serikali inahangaika kupata mnada wa chai katika ukanda huu badala ya kufanyika Mombasa nchini Kenya.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah(wapili kushoto) akikabidhi cheti bwana Thiemo Msewa(kulia) katika hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NOSC, Bwana Filbert Kavia. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri 
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah akizungumza jambo wakati wa hafla hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. 
Operation Director wa Wood foundation Tanzania Bwana Mathew Ng’enda(watatu kushoto) akishangilia mara baada ya wakulima kuwasilisha mada mbalimbali juu ya elimu ya kilimo cha chai (farmer field school) waliyoipata kutoka Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah. na watatu kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NOSC Bwana Filbert Kavia. 



Hivyo makala Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC

yaani makala yote Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/wakulima-206-wapata-mafunzo-ya-kilimo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC"

Post a Comment

Loading...