Loading...

WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

Loading...
WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE
link : WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

soma pia


WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.

WAZIRI Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa wote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.

Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratan vyenye thamani ya shilingi milioni 98  ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.

“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka  vituo vya Afya vya Serikali  524  viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia  wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini  kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya  265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi  kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za  kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343  hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.

“Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam .
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya afya,Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Hivyo makala WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE

yaani makala yote WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/waziri-ummy-awataka-waganga-wakuu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE"

Post a Comment

Loading...