Loading...

Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott

Loading...
Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott
link : Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott

soma pia


Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeupongeza mfuko wa Abbott kutokana na juhudi kubwa za kusaidia kuboresha huduma ya afya katika sekta ya afya nchini.

Kauli hiyo imetolewa Leo na Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu kabla ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto 139 wanaoishi katika mazingira magumu.Mfuko huo kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na benki ya ABC, leo wamekabidhi kadi kwa watoto hao kupitia Waziri Ummy Mwalimu.

“Napenda kuupongeza Mfuko wa Abbott kwa kuwezesha watoto hawa 139 kupata kadi za bima ya afya, hongereni sana. Nimeambiwa Kadi hizi mmezilipia na zitaisha baada ya mwaka mmoja, hivyo naomba muendelee kuzilipa endapo haitawezekana Serikali italipa, lakini naamini kwamba hamtashindwa kuendelea kuiunga mkono Serikali,” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Baada ya Waziri huyo kutoa kauli hiyo, Mkurugenzi wa Miradi endelevu wa Mfuko wa Abbott, Dkt. Festo Kayandabila alisema kuwa wako tayari kuwasaidia watoto hao.Mfuko wa Abbott umekuwa ukiisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili katika juhudi zake za kuboresha huduma za afya. Mfuko huo umesaidia kukarabati Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali pamoja na kukarabati Jengo la maabara kuu.
Mkurugenzi wa Miradi Endelevu wa Mfuko wa Abbott, Dkt. Festo Kayandabila akieleza jinsi mfuko wa Abbott ulivyoshiriki kuwapatia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kadi za bima ya afya. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya ABC, Joyce Malai na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Kurasini, Rabikira Mushi.


Hivyo makala Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott

yaani makala yote Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/waziri-wa-afya-aupongeza-mfuko-wa-abbott.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri wa Afya Aupongeza Mfuko wa Abbott"

Post a Comment

Loading...