Loading...
title : Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo.
link : Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo.
Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo.
Na Kijakazi Abdalla - Maelezo Zanzibar. 17/11/2017.
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Maudline Cyrus Castico amesema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kabla ya kufika wakati (watoto njiti) Zanzibar imeongezeka kutoka 206 mwaka 2016 hadi kufikia 335 kwa mwaka 2017.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto njiti Duniani huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni, Waziri Castico alisema kuwa idadi hiyo ni ya kutisha hivyo jamii inapaswa kufanya juhudi kupunguza tatizo hilo .
Alisema ongezeko hilo la watoto njiti limekuwa likisababisha vifo vingi vya watoto wachanga hasa ndani ya siku saba za awali baada ya kuzaliwa.
Aliipongeza Wizara ya Afya kwa kuchukuwa juhudi kubwa za kuboresha huduma za afya kwa mama na watoto ambapo hivi sasa huduma hizo zinapatikana kila pahala mijini na vijijini.
Alizitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na kuongeza wataalamu na vifaa muhimu za kuhudumia mama wajawazito na wakati wa kujifunguwa pamoja na kusisitiza umuhimu wa kunyonyesha ziwa la mama pekee kwa muda wa miezi sita.
Hata hivyo alisema kuwa katika kuhakikisha huduma hizo zinaboreshwa kwa watoto njiti, Wizara imefanikiwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoshughulikia watoto hao na kwa wazazi.
Alisema jumla ya wafanyakazi 300 wamepatiwa huduma za watoto njiti Unguja na Pemba ili kuhakikisha watoto hao wanakuwa katika mazingira ya afya bora.
Mapema Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema kuwa sababu kubwa zinazopelekea kuzaliwa watoto njiti ni pamoja na msongo wa mawazo wakati wa ujauzito, kujifungua katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 40.
Aliwataka kinababa kuongeza mapenzi kwa wake zao wakati wa ujauzito na kuacha kuwatelekeza ili kumpa nafasi kujifungua akiwa salama na mtoto mwenye afya nzuri.
“Kuna baadhi ya kinababa wanapogundua wake zao wanaujauzito huona ndio fursa ya kutafuta mke mwengine na kumuongezea mke mkubwa matatizo zaidi,’’ alisema Naibu Waziri wa Afya.
Alisema kizazi cha mtoto njiti ni kizazi hai ambacho kinazaliwa kabla ya kutimia umri wa kuzaliwa hivyo ni muhimu kwa wazazi wote wawili kushirikiana katika malezi kuhakikisha kinakuwa vizuri.
Nao wazazi wenye watoto Njiti wamewashukuru wafanyakazi wa Wizara ya Afya kwa huduma wanazozipata wakati wanapofika vituoni jambo ambalo linawapa faraja ya kuendelea kuwalea watoto wao katika misingi mizuri.
Hata hivyo wamesema wapo baadhi ya watu wanaona kuzaa mtoto akiwana hali kama hiyo ni mitihani jambo ambalo linawatia huzuni sana hivyo wameitaka jamii kuondokana na dhana hiyo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Hivyo makala Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo.
yaani makala yote Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/zanzibar-yaadhimisha-siku-ya-mtoto.html
0 Response to "Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani leo."
Post a Comment