Loading...

BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA

Loading...
BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA
link : BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA

soma pia


BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA




BARAZA mkuu la waislam Tanzania(Bakwata) limeelezea sababu za mufti mkuu Abubakary Zuberi   kudaiwa kutaka  kuondolewa katika madaraka yake hayo.

Pia limesema tume ya kufuatilia mali za waislam tayari  imeshatoa ripoti tatu na bado  inaendelea kubaini mali za waislam zilizopotea kinyemela.

Mwenyekiti wa halmashauri kuu baraza kuu  Bakwata na msemaji  wa Bakwata, sheikh Khamis Mataka wa kwanza kutoka kulia 

Akizungumza jijini Dar es salaam leo  mwenyekiti wa halmashuri kuu baraza kuu  Bakwata na msemaji  wa bakwata, sheikh Khamis Mataka amesema pamoja na mambo  mengine mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji ni miongoni mwa sababu za kuwapo kwa taarifa ya kutaka kumuondoa mufti Zuberi.

Amesema pia kumekuwa na madai ya wafanyakazi wa bakwata makao makuu walia njaa na mgogoro  wa walimu wa sekondari  Bondeni ya mkoani Arusha. 

"Hakuna njama zozote za kumuondoa Mufti madarakani, hakuna ubadhilifu wowote unaotuhumiwa nao na kwa hakika ni kuwa hakuna kipindi chochote ambacho baraza limeimarika na kufanya mambo yake kwa mujibu wa katiba kuliko kipindi hiki, "amesema. 

Amesema baraza hilo ni imara na kwamba linaendelea kuzipatia majibu ya kimfumo changamoto  ilizozikabili kwa muda mrefu. 

Amesema baraza hilo litasimamia falsafa ya Mufti Zuberi ya 'Jitambue, Badilika, Acha Mazoea' katika kusimamia mabadiliko ya kimfumo na kiuendeshaji ndani ya baraza hilo. 

"Wale wote watakaobainika kukwaza juhudi hizi kwa kuzusha fitna na kula njama ya kulivuruga baraza, Bakwata itawachukulia hatua stahiki bila ya kuangalia sura wala nafasi zao katika baraza au katika jamii, "amesema. 

Akizungumzia mafao ya wafanyakazi wa baraza hilo, Sheikh Mataka amekiri kudaiwa sh milioni 176.

Katika hatua nyingine, sheikh Mataka amesema walimu wa shule ya sekondari Bondeni mkoani  Arusha wameshalipwa mishahara yao waliyokuwa wakidai ya miezi miwili. 

"Bakwata inawaomba waislamu kuunga mkono mabadiliko ya kimfumo na kiutawala yanayoendelea ndani ya Bakwata kupitia mamlaka mbalimbali  za kikatiba zilizopo, "amesema. 

Amesema kutimia kwa mabadiliko hayo kutaliwezesha baraza hilo kujitegemea, kuimarika kiutendaji na kuwahudumia waislamu na taifa kwa  namna inayostahili.
Na Salha Mohamed, Dar es salaam


Hivyo makala BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA

yaani makala yote BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/bakwata-yakana-uvumi-wa-kuondolewa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BAKWATA YAKANA UVUMI WA KUONDOLEWA MADARAKANI KWA MUFT MKUU WA TANZANIA"

Post a Comment

Loading...