Loading...

Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa

Loading...
Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa
link : Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa

soma pia


Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa

Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kidini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 (Societies Act) inazikumbusha Jumuiya zote zilizosajiliwa chini ya Sheria hii, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria pamoja na masharti ya usajili waliopewa wakati wa usajili. Miongoni mwa masharti yanayopaswa kuzingatiwa na Jumuiya hizo ni pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya Katiba zao ambazo pamoja na mambo mengine  hueleza malengo ya Jumuiya husika.


Hata hivyo, baadhi ya Jumuiya  zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili. Mathalani hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao kwani hakuna Jumuiya yoyote iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Jumuiya ili kufanya kazi za siasa. Tabia hii ni kwenda kinyume na malengo na ni ukiukaji Kanuni ya 7 ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya Sheria ya Jumuiya, inayotamka, kati ya mengine  kwamba Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya malengo yake bila ya kibali cha Msajili’’.  

Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote zinazofanya kazi kinyume na malengo yaliyoainishwa katika Katiba zao zilizosajiliwa kuacha kufanya hivyo mara moja. Aidha Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuia zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika.

Imetolewa na:
Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu)
KATIBU MKUU
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Hivyo makala Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa

yaani makala yote Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/jumuiya-za-kidini-zatakiwa-kuzingatia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa"

Post a Comment

Loading...