Loading...

Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho.

Loading...
Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho.
link : Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho.

soma pia


Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho.

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa awali kesho Disemba 5 wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP dhidi ya Rwanda katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 8:00 za mchana.
Zanzibar Heroes wanashuka dimbani huku kikosi kizima kikiwa katika hali nzuri ambapo ripoti ya Kocha imesema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ana majeraha yatakayomzuia kucheza mchezo huo muhimu kwao.

“Kikosi kizima kipo sawa hatuna majeruhi yoyote, na tumefanya mazoezi mepesi katika uwanja Machakos Girl High School kwa ajili ya mchezo huo, tunawaheshimu Rwanda hasa wakiwa katika Katika Mashindano haya ni timu nzuri na tunatarajia kushuhudia mchezo mzuri kwa kila upande”. Alisema Kocha mkuu Hemed Suleiman (Moroco).

Katika mchezo huo Heroes inawategemea zaidi viungo 

wake mahiri Mudathir Yahya wa Singida United na Mohd 

Issa "Banka" wa Mtibwa Sugar.

Benchi la ufundi la Hereos linaongozwa na Hemed Suleiman “Morocco” (Kocha Mkuu), Hafidh Muhidin (Msaidizi), Ali Suleiman “Mtuli” (Msaidizi), Abdulwahab Dau (Meneja), Saleh Ahmed “Machupa” (Kocha wa Makipa)na Abrahmani Ali (Mtunza vifaa).

Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-
WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).
WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).
WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Heroes wapo kundi A pamoja na Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.


Hivyo makala Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho.

yaani makala yote Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kikosi-cha-zanzibar-heroes-wapo-tayari.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kikosi cha Zanzibar Heroes Wapo Tayari Kuivaa Timu ya Rwanda Kesho."

Post a Comment

Loading...