Loading...
title : MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM
link : MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM
MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM
Na Dotto Mwaibale
VILIO Majonzi na simanzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.
Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani."Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.
Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.
Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.
Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.
Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mamia-wamuaga-mwanahabari-joyce-mmasi.html
0 Response to "MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment