Loading...
title : MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO
link : MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO
MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao.
Amesema elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi.Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa, Lindi.Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la kwanza.
“Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani faida watakuja kuiona baadaye.”Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao.
Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. “Wote ni mashahidi watoto wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.”Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala ya kuwaachia walimu peke yao.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa, Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na watoto wakati alipotembelea bwalo la chakula la Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa katika mahafali ya shule hiyo, Desemba 2, 2017.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti kwa mhitimu wa Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2, 2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
Baadhi ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo Desemba 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Hivyo makala MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO
yaani makala yote MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mary-majaliwa-wazazi-wekezeni-kwenye.html
0 Response to "MARY MAJALIWA: WAZAZI WEKEZENI KWENYE ELIMU YA WATOTO"
Post a Comment