Loading...

Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.

Loading...
Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.
link : Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.

soma pia


Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.

Mwambawahabari

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa.

Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.

Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.

Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.

Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.

“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili, hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha yetu” amesema Meya Mwita.

Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.

Imetolewa leo Desemba 1 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda Hamidani Magoma mwenyemiwani  walipokutana katika ofisi za Mastahiki Meya jiji.

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda  wa Mayotte Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita watatu kulia mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Kisiwa Cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa walipomtembelea ofisini kwake.
Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda  wa Mayotte Nchini Ufaransa Hamidani Magoma akimuelekeza jambo kwenye kwenye dokomenti Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita walipomtembelea ofisini kwake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya biashara jijini hapa.



Hivyo makala Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.

yaani makala yote Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/meya-mwita-ashangaa-watu-wa-kisiwa-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili."

Post a Comment

Loading...