Loading...
title : OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
link : OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amesema, kutokana na mchango mkubwa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika maendeleo ya kiuchumi, usalama, utawala wa sheria na utawala bora, Kuna umuhimu wa Serikali kuendelea kuiimarisha Ofisi hiyo.
Ameyasema hayo wakati akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Profesa Palamagamba Kabudi kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uzinduzi wa baraza hilo umefanyika siku ya jumatatu katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la LAPF Mkoani Dodoma.
Uzinduzi wa Baraza hilo, ulitanguliwa na uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi. Zoezi la uchaguzi lilisimamiwa na Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya, Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Bi. Jane Mbura na Afisa Kazi Bi. Razina Tuusa. Waliochaguliwa kwa kura za Siri ni Wakili wa Serikali Mkuu Monica Mbono ambaye anakuwa Katibu na Bw. Michael Masanja anakuwa Katibu msaidizi.
Mhe. Masaju akiwa ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi, ameyataja maeneo ambayo Serikali inatakiwa kuendelea kuyaimarisha katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ni pamoja na, Raslimali fedha, mafunzo, makazi salama kwaajli ya mawakili wa serikali na miundombinu ya ofisi.
“Mhe. Waziri, yapo masuala ya kisera ambayo tunaomba Serikali inayashughulikie ipasavyo ili kuiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Maeneo hayo ni kuajiri Mawakili wa Serikali na Watumishi wa Kada zingine, kujenga majengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika Ofisi za Wilaya na Mikoa ili kuokoa fedha inayotumika kulipia pango”. Ameleza Mwanasheria Mkuu.
Kwa upande wa mafunzo, Mwanasheria Mkuu, ameishauri Serikali katika kuwajengea uwezo wa kitaalam Mawakili wa Serikali na watumishi wenzao katika maeneo ya kipaumbele na kuimarisha maslahi ya mawakili wa serikali na watumishi wote katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu akimkaribisha Mhe Waziri wa Katiba na Sheria kuzindua Baraza la Wafanyakazi na katika salamu zake alisema ni muhumu kwa Serikali kuendelea kuiimarisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kutokana na umuhimu wake katika maendeleo ya nchi, kiuchumi, kiusalama, katika utawala wa sheria na katiba
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Profesa Paramagamba Kabudi akitabasamu mara baada ya kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali siku ya jumatatu. Baraza hilo linakutana kwa siku mbili katika ukumbi wa LAPF mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo, wajumbe wa Baraza ni pamoja na Mawakili Wafawidhi wa Serikali, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Wajumbe wa TUGHE na mada mbalimbali zilitolewa wakati wa uzinduzi hao.
Hivyo makala OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
yaani makala yote OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/ofisi-ya-mwanasheria-mkuu-wa-serikali.html
0 Response to "OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI"
Post a Comment