Loading...

SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA.

Loading...
SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA.
link : SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA.

soma pia


SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA.


Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega jana amekamata samaki aina ya sangara wachanga na wazazi tani 11 waliokuwa wakitoroshwa kwenda nchi jirani ya DRC kwa kukwepa kulipa kodi.

Samaki hao tani 11 walitakiwa kulipiwa ushuru wenye thamani ya Tsh.99,000,000, badala yake wafanyabiashara hao wa kikongo walikwepa kulipa ushuru huo kwa kuchukua kibali kinachoonesha samaki hao wanaenda kuuzwa Tunduru mkoani Ruvuma

Akizungumza na uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe Ulega amesema kuwa watumishi wa serikali watangulize Uzalendo katika nafasi zao wanazozitumikia kuliko kuendekeza rushwa."Jamani naombeni sana msimamieni sheria Ili kulinda Rasilimali zetu zisitoroshwe kwenda nje bila kulipiwa Kodi,tumuunge Mkono Rais wetu John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Rasilimali hizi zinawanufaisha wananchi na sio watu wachache"alisema.

Ulega aliesma ni kinyume cha sheria kuvua samaki wachanga na wazazi, na ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Ilemela kwa kupitia Mkurugenzi wake kuhakikisha wanasimamia sheria ipasavyo na hakuna samaki wachanga na Wazazi kuvuliwa.

"Ikitokea wakati wa ukaguzi wenu mmekamata samaki wachanga au wazazi taifisheni na sheria ichukue mkondo wake kwa yoyote anayehusika au anayevunja sheria kwa kujua au kutokujua"alisema Ulega.Katika hatua nyingine Mhe. Naibu Waziri Abdalla Ulega alipata fursa ya kuhutubia wafanyabishara katika soko hilo,mara nyingi Naibu Waziri alikatishwa hotuba yake kwa kushangiliwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo.

Aidha wafanyabiashara hao walimweleza Naibu Waziri changamoto wanazokumbana nazo hapo sokoni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama na ubovu wa miundombinu ya vyoo katika soko hilo.

Mhe.Ulega amempa siku tatu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kuhakikisha maji na miundombinu ya vyoo sokoni hapo inashugulikiwa ndani ya siku tatu."Mkurugenzi nakuagiza kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hili viwe vimepatiwa Ufumbuzi".Alisema Ulega.
 .Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akipima ulefu mmoja wa Samaki waliokamatwa tani 11 wakisafirishwa kinyume na taratibu mkonani katika soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa  Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akifafanua jambo mbele ya watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na wafanya biashara wa katika  soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akiwa akisalimiana na wafanyabiashara katika soko hilo. Picha  zote  na Emmanuel Massaka,MMG Mwanza.

.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akikagua miundo mbinu ya maji katika soko hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hilo viwe vimepatiwa Ufumbuzi


Hivyo makala SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA.

yaani makala yote SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/samaki-wachanga-na-wazazi-zakamatwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SAMAKI WACHANGA NA WAZAZI ZAKAMATWA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA MWALONI JIJINI MWANZA."

Post a Comment

Loading...