Loading...

SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE

Loading...
SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE
link : SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE

soma pia


SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE

Serikali imesaini Mkataba wa makubaliano wa Miradi ya Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women). Akitia saini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Mkataba huo unahusu Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Wanawake Watanzania.

Bibi Sihaba Nkinga ameongeza kuwa Mkataba huo umeainisha maeneo ya ushirikiano ambayo ni Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW),Kufanya Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000, Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2021).

Aidha Bibi Sihaba Nkinga amesisitiza kuwa Mkataba huo utasaidia kuendeleza jitihada za Serikali ya Tanzania na Wadau mbalimbali katika kufikia Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. “ Makubaliano haya yatasaidia sana katika kusaidia juhudi za Serikali na Wadau kumuwezesha wanawake wa Tanzania kujikwamua kiuchumi na kufikia usawa wa kijinsia”alisema Bibi. Sihaba.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UN Women - Tanzania, Bibi Hodan Addou amesema kuwa pamoja na jitihada zilizofanyika kati ya Shirika hilo na Serikali katika kuwaletea Maendeleo Wanawake, jitihada zingine zitakazofanyika ni kusaidia juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kuongeza Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na kutoa maamuzi kwenye ngazi zote.

“Tunaahidi kushirikiana naSerikali katika kumuinua na kumuendeleza mwanamke wa Kitanzania katika kujikwamua kiuchumi” alisema Bibi Hodan. Mkataba huo wa Mwaka mmoja (2017/2018) unalenga kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kujiajiri, kujitegemea na hivyo kujikwamua kiuchumi kwa kujiongezea kipato binafsi, familia na taifa kwa ujumla.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Bibi. Hodan Addou (kulia) wakitia saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya Wanawake utakaodumu kwa kipindi cha Mwaka mmoja (2017/2018) katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Desemba 05, 2017.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Bibi. Hodan Addou (kulia) wakikabidhiana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya Wanawake utakaodumu kwa kipindi cha Mwaka mmoja (2017/2018) katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Desemba 05,2017.


Hivyo makala SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE

yaani makala yote SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/serikali-yasaini-mkataba-wa-ushirikiano.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE"

Post a Comment

Loading...