Loading...
title : SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI
link : SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI
SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesisitiza kuanzishwa kwa mtaala wa elimu ya fedha mashuleni ili kuwajengea uwezo vijana wa kujua na kutambua kujua matumizi sahihi ya fedha. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 21, 2017) wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Akizindua mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022, Waziri Mkuu alisema uwepo wa miundombinu muhimu iliyojengwa na inayojengwa na Serikali; na sekta binafsi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini; na ongezeko la watumiaji wa mitandao ya simu na huduma za mawasiliano ni kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo.
“Kati ya fursa nzuri iliyotajwa kwenye mpango huo ni uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi. Tukijenga vizuri juu ya misingi hii tunaweza kupiga haraka hatua za maendeleo katika sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla wake,” alisema.
Alisema ameupitia mpango huo na kubaini kuwa umeainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hii katika harakati zake za kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. Hata hivyo, Waziri Mkuu alikiri kuwa mpango huo umeainisha fursa ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kuongeza matumizi ya huduma za kifedha.
“Changamoto zilizoainishwa ni pamoja na kuimarisha utawala wa matumizi ya fedha taslimu kwa ajili ya malipo badala ya matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya malipo; kukosekana kwa utambulisho wa kipekee (unique identification) kwa Watanzania walio wengi; uhalifu kwa njia za mtandao (cyber-crime); kukosekana kwa mifumo madhubuti ya taarifa za kutosha za watumiaji wa huduma za fedha na dhamana zao; na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha,” alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amenyanyua kitabu cha mpango kazi wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, mwingine kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitambu cha mpango kazi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James wakati wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kitabu cha mpango kazi, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Gavana Mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof Florens Luoga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Benno Ndulu wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Picha zote na KAJUNASON/MMG.
Hivyo makala SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI
yaani makala yote SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/serikali-yasisitiza-elimu-ya-fedha.html
0 Response to "SERIKALI YASISITIZA ELIMU YA FEDHA ITOLEWE MASHULENI"
Post a Comment