Loading...
title : TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar
link : TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar
TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar
MTANDAO wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na African Population and Health Research Center (APHRC) umekutana na wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho cha majadiliano kilichoshirikisha viongozi kama wabunge, madiwani wa maeneo hayo pamoja na watendaji wa sekta ya elimu, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao alisema kikao hicho kinajadiliana namna ya kutekeleza mradi huo utakao lenga kuboresha elimu.
Akifafanua zaidi, Bi. Sekwao alisema kikao hicho kitaangalia matatizo gani kielimu yanayowakwaza watoto wanaoishi katika miji na majiji yenye msongamano wa makazi kiujumla na kuangalia namna wanaweza kukabiliana nayo. Alisema mradi huo utakuwa wa miaka miwili lakini baadaye unaweza kuwa endelevu kadri ya mahitaji yake kwa jamii husika.
Akichangia katika kikao hicho, Mthibiti Ubora wa Shule Wilaya za Temeke na Kigamboni, Mashaka Munjalloh alisema mradi huo utawasaidia watoto kutoka maeneo yenye msongamano kupata elimu bora itakaowasaidia katika maisha yao.
Wapili kulia ni Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akichangia mada katika kikao cha wadau wa elimu jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kutekeleza mradi wa kusaidia maboresho ya elimu kwa makazi yenye msongamano wa watu mkoani Dar es Salaam. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea.
Hivyo makala TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar
yaani makala yote TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/tenmet-aphrc-wakutana-na-wadau-wa-elimu.html
0 Response to "TENMET, APHRC wakutana na wadau wa elimu kujadili changamoto za elimu kwenye msongamano wa makazi Dar"
Post a Comment