Loading...

Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

Loading...
Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.
link : Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

soma pia


Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

Na Shamimu Nyaki – WHUSM.

Serikali imewataka wasanii kutengeneza kazi nzuri zenye ubora zinazozingatia maadili ya Kitanzania ili kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kudhamini kazi hizo katika kuziandaa na kuzisambaza.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akizindua Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo ambapo ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuamua kuchukua dhamana ya kusambaza kazi za wasanii ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za wasanii hao kupitia njia mbalimbali walizokuwa wanatumia wasanii hao ambazo zilikua zikiwalipa kiasi kidogo.

“Nimefurahishwa sana na Mfumo huu namna ambavyo utaweza kutatua changamoto ya wizi wa kazi za wasanii wetu kwa vile umeonyesha wazi namna ambavyo msanii anaweza kunufaika na kazi yake kuanzia idadi ya kazi zake zilizoenda sokoni,asilimia anazopata kwa kazi yake ambayo ni kuanzia 40-50 pamoja na kumuwezesha kutouza Haki Miliki yake kama walivyokuwa wanafanya hapo awali.”Alisema Mhe.Mwakyembe.

Aidha amewataka Wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitakidhi vigezo vyinavyotakiwa na Kampuni hiyo ambapo pia ameiagiza Kampuni hiyo kutochukua kazi yeyote ambayo itakuwa haina ubora wala kuwa na maadili.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) pamoja na viongozi wa Kampuni ya MaxMalipo wakionyesha baadhi ya kazi za wasanii zitakazosambazwa na Kampuni hiyo kupitia mfumo wa MaxBurudani leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa MaxBurudani ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo wenye lengo la kusambaza kazi za wasanii.



Hivyo makala Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

yaani makala yote Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/wasanii-watakiwa-kutengeneza-kazi-nzuri.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wasanii watakiwa kutengeneza kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini."

Post a Comment

Loading...