Loading...
title : WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI
link : WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI
WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI
Watendaji na wataalamu wa Wilaya ya Handeni wametakiwa kusimamia na kuweka suala la elimu ya madhara ya ukeketaji kuwa ajenda rasmi kwenye vikao vyao ngazi ya Kata na Tarafa ili kukomesha kabisa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike wa jamii ya wafugaji hususani pindi mradi wa “KIJANA WA LEO” unaofadhiliwa na shirika la Amref kukoma.
.Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ametoa rai hiyo leo alipohudhuria sherehe za uvushwaji rika wa wasichana 170 wa jamii ya wafugaji(Ndito) zilizofanyika Kata ya Malezi katika mtaa wa Kwamadule.
Mh. Gondwe alisema kuwa ni haki ya binti anapokuwa mtu mzima na kuvushwa rika asiweze kunyanyaswa kijinsia, kwasababu athari za ukeketaji zinafahamika ikiwa ni pamoja na kuwa ni kitendo ambacho ni kinyume na maagizo ya Mungu lakini pia uvunjwaji wa haki za binadamu..
Ameongeza kuwa jamii ya wafugaji inatamaduni zilizoshiba na wanachangia kwa kiasi kikubwa kuingizia pato na fedha za kigeni Taifa, ni utamaduni bora unaotambulisha Tanzania kwa zaidi ya makabila 120.Watu wanapenda tamaduni za kimasai na jamii za wafugaji wengine lakini mila ambazo ni potofu zinazoleta maumivu katika jamii zitokomezwe.
“ sherehe na kila kitu kifanyike, watoto wafundishwe lakini ukeketaji hapana ili tumuokoe binti huyu na maumivu makali kwa sababu morani wamekubali kuoa wananwake ambao hawajakeketwa na kwasasa wanaoa hata jamii zingine ambazo wanawake hawajakeketwa” alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni akizungumza na Mangariba na kuwapongeza kuelimika kuacha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike.
mmoja wa wsichana waliovushwa rika bila kukeketwa akipokea cheti cha kufuzu mafunzo ya kuzuia ukeketaji na mafunzo ya afya ya uzazi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akikaribishwa kwenye sherehe za uvushaji rika.
mangariba wakionesha namna ambavyo huwakamata wasichana (ndito) wa kimasai kuwapeleka kwenye chumba cha ukeketaji.
Mmoja wa wazee wa kimila akishukuru Amref kwa Elimu waliyopewa juu ya uvuhsaji rika wasichana kwa kufanya sherehe na mila zao bila kukeketa.mangariba wakionesha namna ambavyo huwakamata wasichana (ndito) wa kimasai kuwapeleka kwenye chumba cha ukeketaji.
mmoja wa wsichana waliovushwa rika bila kukeketwa akipokea cheti cha kufuzu mafunzo ya kuzuia ukeketaji na mafunzo ya afya ya uzazi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI
yaani makala yote WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/watendaji-na-wataalamu-wa-wilaya-ya.html
0 Response to "WATENDAJI NA WATAALAMU WA WILAYA YA HANDENI WATAKIWA KUSIMAMIA SUALA LA ELIMU YA MADHARA YA UKEKETAJI"
Post a Comment