Loading...
title : WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO
link : WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO
WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa kukamata mifugo kiholela na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria huku akisifu utendaji kazi ya wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa sheria za mifugo nchini.
Mpina ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Handeni ambapo alitumia fursa hiyo kupiga marufuku ukamataji mifugo kiholela huku akimtaja Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Gondwe kama kielelezo cha kuwa kiongozi wa kwanza kitaifa anayezifahamu vizuri na kuzisimamia kikamilifu sheria za mifugo na kuleta tija katika ukuaji wa sekta hiyo ikiwemo kuanzisha kijiji cha wafugaji,kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na utoaji huduma bora za mifugo wakati wote.
Akizungumzia tatizo hilo la ukamataji holela wa mifugo nchini, Waziri Mpina amesema kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na Serikali kuamua kuagiza kutoka nje ya nchi basi ingezilazimu kutumia kiasi cha sh. Trilioni 17.8 huku kaya milioni 4.49 za kilimo nchini zinajishughulisha na ufugaji mifugo aina mbalimbali.
“Watendaji wa Serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki salama, tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria”alisema.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kulia akitazama mifugo ya ng'ombe aina ya Borani waliyopo kwenye ranchi ya mzeri wilayani Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe kushoto akimueleza jambo WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kulia ambaye alifanya ziara ya kikazi wilayani humo
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati alipoitembelea ranchi ya mzeri wilayani humo.
Hivyo makala WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO
yaani makala yote WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/waziri-mpina-awakaanga-viongozi.html
0 Response to "WAZIRI MPINA AWAKAANGA VIONGOZI WANAOHUJUMU WAFUGAJI,AMSIFU DC GONDWE KUSIMAMIA KIKAMILIFU SEKTA YA MIFUGO"
Post a Comment