Loading...
title : BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA
link : BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA
BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA
Na Nyakongo Manyama
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na wabunifu wa Tanzania wamezindua Chama cha Mitindo Tanzania (FAT) kitakachowaunganisha wabunifu wote hatua inayolenga kuinua na kuiongezea hadhi sekta ya mitindo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza amesema sekta ya mitindo nchini ikiimarishwa itaweza kuleta mapinduzi makubwa kwa kuzalisha ajira kwa vijana.
“Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujenga Tanzania ya viwanda, tasnia ya ubunifu wa mavazi, tumeamua kulima pamba ambayo ndiyo itakayozalisha mavazi, hivyo kusingekuwa na wabunifu hatungekuwa na mavazi yenye utamaduni wa Tanzania”
Aidha Mngereza aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa ngozi duniani, ambapo katika kutumia fursa hiyo, Chama cha wabunifu Tanzania kimepanga raslimali hiyo kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu, mikanda na mabegi .
Naye mwanzilishi wa chama hicho Bw. Mustafa Hassanali amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni katika kukuza, kuimarisha na kuendeleza sekta ya mitindo Tanzania pamoja na kuwapatia ujuzi, uzoefu wadau wote wa sekta ya mitindo Tanzania.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania, Adrian Nyangamalle amekipongeza chama hicho na kusema kuwa tasnia ya mitindo imetoa ajira kubwa kwa vijana na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano na jumuiya hiyo ili kutimiza malengo yake kwa haraka.
Aidha Nyangamalle ameongeza kuwa Shirirkisho la Chama cha Ufundi kwa kushirikiana na BASATA wameanzisha mchakato wa kuwatambua wasanii wote nchini kwa kuandaa kanzi data itakayosaidia kufahamu wasanii waliopo nchini ili kuweza kutambulisha mchango wao katika kuinua uchumi.
Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Adrian Nyangamalle na kushoto ni Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous
Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (wa pili kulia) akizindua Chama cha Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam
Hivyo makala BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA
yaani makala yote BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/basata-yazindua-chama-cha-wanamitindo.html
0 Response to "BASATA YAZINDUA CHAMA CHA WANAMITINDO TANZANIA"
Post a Comment