Loading...
title : BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU
link : BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU
BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU
Na Veronica Simba – Dodoma
Serikali imebainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 499 zimeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme nchini kote katika mwaka huu wa fedha unaoendelea.
Hayo yalisemwa jana, Januari 24 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa katika ziara katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini kwa ajili ya kujionea hali ya upatikanaji wa nishati hiyo muhimu pamoja na kuzungumza na wananchi.
Naibu Waziri Mgalu, ambaye aliambatana na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde aliwaambia wananchi wa maeneo aliyotembelea kuwa, kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na kitawezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme katika vijiji vyote 7873 vilivyosalia nchi nzima.
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli pamoja na Bunge la Jamhuri kutuidhinishia kiasi hicho cha fedha. Kazi yetu sisi wasaidizi wake katika Wizara ya Nishati ni kuhakikisha tunatekeleza jukumu alilotutuma la kuwapelekea wananchi kote nchini nishati ya umeme wa uhakika. Tunaahidi hilo litafanyika kwa ukamilifu.”
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Chisichili Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme.
Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (aliyesimama), akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (wa pili kutoka kulia), kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) akibadilishana mawazo na wananchi wa Mtaa wa Chisichili, Kata ya Mkonze mkoani Dodoma wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme. Kulia kwake ni Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde.
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
Wananchi wakiuliza maswali na kutoa maoni mbele ya Naibu Waziri Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kujionea hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini.
Hivyo makala BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU
yaani makala yote BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/bilioni-499-zimidhinishwa-kutekeleza.html
0 Response to "BILIONI 499 ZIMIDHINISHWA KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME PEKEE – MGALU"
Post a Comment