Loading...

Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba

Loading...
Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba
link : Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba

soma pia


Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba

Na Maryam Kidiko  -  Maelezo Zanzibar 
                               
KATIBU Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Mussa Tafurwa alisema chama hicho kinatarajia kufanya Mikutano ya kanda ya Unguja na Pemba tarehe 27-28  mwezi huu.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na Waandishi wa habari  Ofisini kwake Kijagwani Mjini Unguja. alisema Unguja mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa  kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo na Pemba Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Madungu.

Alisema kuwa Mikutano hiyo ya siku mbili itajadili  shughuli mbali mbali ikiwemo kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kanda,Wajumbe wa Baraza kuu Taifa,Wajumbe wa mkutano mkuu Taifa na Wajumbe wa kamati Tendaji.

Kwa upande wa  mkutano mkuu wa Chama utafanyika tarehe 10-11 Febuari mwaka huu katika Ukumbi wa Baraza la Wawaklishi la zamani Kikwajuni na kujumuisha wageni mbali mbali wa ndani na nje ya Nchi.

Aidha alisema Mkutano utajadili taarifa mbali mbali sambamba na kufanya uchaguzi Mkuu wa Rais wa Chama, Makamo wa Rais, Wajumbe wa kamati tendaji wa Taifa.

Pia watachaguliwa Wajumbe wa kukiwakilisha chama kwenye Baraza kuu la shirikisho la vyama vya Wafanyakazi na Wajumbe wa kukiwakilisha chama katika mkutano mkuu wa shirikisho.

Akiongezea zaid alisema kuwa katika mkutano huo anaetarajiwa kuwa mgeni rasmin ni Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Zaidi ya Wageni 180 wanatarajiwa kuhudhuria kutoka Tanzania,Kenya,Uganda pamoja na Rwanda ambapo Kauli mbiu ya Mkutano huo ni Uhuru katika kufundisha kumjenga Mwalimu.


Hivyo makala Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba

yaani makala yote Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/chama-cha-walimu-zanzibar-zatu-kufanya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) kufanya mkutano wake kesho kwa kanda ya Unguja na Pemba"

Post a Comment

Loading...