Loading...
title : DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO
link : DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO
DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe ameagiza kukamatwa kwa viongozi wote waliofuja shilingi milioni 32 za ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Idibo.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo lililokwenda sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.Mhe. Mchembe aliwaomba TAKUKURU kuwakamata viongozi wote wanaosimamia ujenzi wa shule ili waweze kuhojiwa matumizi ya pesa na wizi uliotokea tokea kuanza kwa ujenzi huo.
"Nimepokea taarifa ya Kamati ya Ujenzi ambayo imebaini wizi wa shilingi milioni 12 na matumizi ya utata yenye thamani ya shilingi milioni 20, hivyo ninawaagiza TAKUKURU na OCD ndani ya siku saba kuwakamata wale wote wanaohusika na sheria ichukue mkondo wake," alisema Mhe. Mchembe.
Aidha mpaka sasa japo kuna dosari Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Idibo umemaliza madarasa 3, vyoo na jengo la utawala.Wakati huo huo Mhe. Mchembe alikabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupanua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita na OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu (kulia) wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo, shule ya sekondari ya kata ya Idibo sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (wa kwanza kulia) akabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa Jeshi la Polisi na uongozi wa kata ya Idibo kwa ajili ya kupaua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.
Hivyo makala DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO
yaani makala yote DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dc-gairo-aamuru-kukamatwa-viongozi_8.html
0 Response to "DC GAIRO AAMURU KUKAMATWA VIONGOZI WALIOKULA FEDHA ZA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA IDIBO"
Post a Comment