Loading...
title : DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO
link : DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO
DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amewaasa Wanafunzi wanaosoma masuala ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha Uhasibu TIA Kuwa Wazalendo pindi wanapofika katika maeneo yao ya kazi ili wawe mfano bora kwa Taifa.
Dc Lyaniva ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya Masuala ya ununuzi na Ugavi,yaliyoandaliwa na Bodi ya PSPTB kwa wanafunzi wa Chuo cha TIA ambao wanasoma masuala ya manunuzi.
"Msiwe na mawazo ya kufikiria kupata pesa za haraka haraka pindi mnapopata kazi,kwani mkiwa na moyo huo mtaangukia katika makosa ya uhujumu Uchumi ,jambo ambalo watu wengi wa taaluma yenu mwisho wa siku wamekuwa wakiangukia Polisi"amesema Dc Lyaniva.
Ameaongeza kwa kusema kuwa anapenda kuwambia kwamba Maadili yenye Uzalendo ndio nguzo ya Msingi katika kufanya kazi, ndio Maana Rais wetu Dk John Magufuli amefanikiwa kubadilisha mambo mengi katika nchi kutokana na uzalendo wake.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha TIA Kampasi ya Dar es Salaam, wanaosoma Masuala ya Manunuzi wakati wa Semina Maalum iliyoandaliwa na bodi ya Wataalam wa Manunuzi PSPTB
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Wataalam wa Manunuzi nchini, Godfred Mbanyi akizungumza na Wanafunzi wa Chuo cha uhasibu cha TIA ambao walikuwa wanapata Semina Maalum juu ya masuala ya Manunuzi.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu TIA, Mugisha Kamala akizungumza kwa ajili ya kuwakaribisha wageni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke katika Semina hiyo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi
Sehemu ya Wanafunzi waliohudhuria Mafunzo ya masuala ya Ununuzi na Ugavi kutoka PSPTB yaliyoendeshwa katika Chuo cha uhasibu TIA.
Hivyo makala DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO
yaani makala yote DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dc-lyaniva-awaasa-wataalamu-wa-manunuzi.html
0 Response to "DC LYANIVA AWAASA WATAALAMU WA MANUNUZI KUWA WAZALENDO"
Post a Comment