Loading...

DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA

Loading...
DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA
link : DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA

soma pia


DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Sophia Mjema amefanya ziara ya kukagua ukarabati wa majengo unaofanyika kwenye Sekondari ya Wasichana Jangwani na Sekondari ya Wavulana Azania ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 3.

Amefafanua kiasi hicho cha fedha pia kinahusisha ukarabati wa sekodari ya Pugu na unafanywa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania(TBA).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, akiwa Jangwani ambayo alisoma kidato cha tano na sita, Mjema amesema amefanya ziara hiyo kuangalia maendeleo ya ukarabati huo.

"Nitumie nafasi hii kuwapongeza Wakala wa Majengo kwa kazi nzuri wanayoifanya.Pia naomba ukarabati huu uende kwa haraka kama ambavyo imeagizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,"amesema.

Amefafanua ukarabati huo umeleta mabadiliko makubwa katika shule hiyo hasa walipokarabati vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu  ambavyo hapo awali havikuwepo Jangwani.

"Kwa ukarabati huu hata wanafunzi wenye uhitaji maalumu wanaweza kuendana na mazingira ya shule kwani yatakuwa rafiki kwao,"amesema.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua Milango ya Choo cha Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani ambayo inakarabatiwa katika mpango maalum wa ulitolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk John Magufuli ya ukarabati wa shule kongwe ambapo ukarabati huo  umegharimu Shilingi Bilioni 3 za kitanzania.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akikagua Mabweni  ya Shule Sekondari ya Wavulana ya Azania ambayo inakarabatiwa na Wakala wa Majengo TBA
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema, akizungumza na Wasichana  wa shule ya Sekondari ya jangwani juu ya kujiepusha ngono wakiwa shuleni ili wasipate Mimba.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo  akisalimiana na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Azania Sekondari Goodlove Kapufi kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa ukarabati wa shule hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema  akikagua mazingira ya shule ya sekondari ya Jangwani,Kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo.


Hivyo makala DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA

yaani makala yote DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dc-mjema-akagua-ukarabati-sekondari-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC MJEMA AKAGUA UKARABATI SEKONDARI YA JANGWANI, AZANIA"

Post a Comment

Loading...