Loading...
title : Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali
link : Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali
Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.
Vyombo vya Habari nchini vimeaswa kuunga mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza Wakati wa ziara yake yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi ya Taifa letu imejengwa katika uchumi jumuishi.
“ Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kueleza faida za miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) kwa wananchi ili nao washiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ambapo ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo” Alisisitza Dkt. Abbasi.
Akifafanua amesema kuwa dhamira yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea kutekelezwa kupitia mfumo wa elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha, Ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli na upatikanaji wa huduma muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ili kuhakiksha kuwa kila mwananchi anapata huduma muhimu na za msingi katika ubora unaotakiwa.
Hivyo makala Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali
yaani makala yote Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/dkt-abbasi-aviasa-vyombo-vya-habari.html
0 Response to "Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali"
Post a Comment