Loading...
title : HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE
link : HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE
HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE
SHULE ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam imeng’ara kwenye matokeo ya darasa la nne kwa kufanikiwa kuwa ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wanafunzi saba kati ya 10 walioingia kumi bora kitaifa.
Katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo pia imefanikiwa kutoa wanafunzi wa kike saba bora kitaifa miongoni mwa wasichana 10 walioingia kumi bora kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa.
Wanafunzi waliofanikiwa kuingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khatibu (Hazina), Fildaus Abbas (Hazina), Martha Shayo (Hazina), Momy Lawrence (Hazina), Zayyana Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Gospel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Nurdin (Hazina), Sharp Gabukambwe (Mungu Bariki) na Muhamed Hoti (Mudio Islamic).
Wasichana walioingia 10 bora kitaifa ni Rahma Khassan (Hazina), Fildaus Msafiri (Hazina), Martha Shayo (Hazina), Momy Laurence (Hazina), Zayyana Nassoro (Hazina), Kokudyness Rweyemamu (Full Goaspel), Jesca Nenula (Hazina), Lailaty Balii (Hazina), Sala Elias (Mwilamvya), Veneranda Richard (Mwilamvya).
Akizungumza, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kwenye kundi la wanafunzi chini ya 40 shule ya Hazina imekuwa ya kwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema shule hiyo imefanikiwa pia kuwa ya tatu kitaifa na ya kwanza kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo wamekuwa wakipata mafanikio makubwa mwaka hadi mwaka kwenye matokeo ya kitaifa.
Alitoa mfano kuwa shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kitaaluma kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na hadi Taifa na kumekuwa na mabadiliko chanya.
Cheche alisema malengo yao ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.
Hivyo makala HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE
yaani makala yote HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/hazina-yangara-tena-matokeo-darasa-la.html
0 Response to "HAZINA YANG’ARA TENA MATOKEO DARASA LA NNE"
Post a Comment