Loading...
title : JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA
link : JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA
JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA
Na Mwandishi Wetu,
09/1/2018 Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umewaahidi watanzania kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kwa mwaka 2018.
Prof. Janabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho alizitaja ahadi zingine ni pamoja na kuendeea kupunguza kupeleka wagonja nje ya nchi, kupunguza gharama za tiba, kuongeza idadi ya huduma, kuboresha usafi katika Hospitali na kuendelea kushirikiana na wananchi.
Mwenyekiti huyo alisema kwa mwaka 2018 wamejipanga kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 64,093 walitibiwa katika Taasisi hiyo kati ya hao wagonjwa wa nje walikuwa 60796 na waliolazwa 3297.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea kuhusu mikakati ya utendaji kazi kwa mwaka 2018 moja ya mkakati huo ukiwa ni kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa kiwango cha kimataifa katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kilichofanyika hivi karibuni. Kulia ni Mwanasheria wa Taasisi hiyo Maulid Kikondo.
Wakurugenzi wa Idara na vitengo vinavyojitegemea vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alielezea kazi zilizofanyika katika Taasisi hiyo kwa mwaka 2017 katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kilichofanyika hivi karibuni. Jumla ya wagonjwa 1025 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kwa mwaka 2017 na hivyo Taasisi kuokoa zaidi ya bilioni 29 ambazo Serikali ingezilipa kama wagonjwa hawa wangefanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi.
Kikao cha kwanza cha Manejimenti cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mwaka 2018 kikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akisoma taarifa za utendaji kazi wa idara yake kwa kipindi cha miezi mitatu katika kikao cha kwanza cha Menejimenti kwa mwaka 2018 kilichofanyika hivi karibuni. Picha na JKCI
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA
yaani makala yote JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/jkci-yawaahidi-watanzania-kuendelea.html
0 Response to "JKCI YAWAAHIDI WATANZANIA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA"
Post a Comment