Loading...
title : KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
link : KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
Na Fredy Mgunda,Iringa
JAMII imetakiwa kuwalea, kuwatunza na kuwajali watu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuhakikisha kwamba wanaishi katika mazingira mazuri, yenye usalama na sio kuwanyanyapaa pale wanapohitaji mahitaji yao ya msingi.
Aidha Chama cha walemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Iringa kimeshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali, ili walemavu hao pia waweze kupata elimu juu ya afya ya usalama wa ngozi pamoja na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao.
Hayo yalisemwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati wakati alipokuwa akitoa msaada wa mafuta maalum ya kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi albino katika hafla fupi iliyohudhuriwa na walemavu hao ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa
“Nampongeza Mwenyekiti wa TAS mkao wa Iringa kwa jitihada zake alizozifanya juu ya namna ya kupata mafuta haya, kama chama endeleeni kuwa wabunifu namna ya kulisaidia kundi hili tete la walemavu kwa kuwalea na kuwatunza katika mazingira mazuri”, alisisitiza mbunge Kabati
Vilevile Kabati aliongeza kwa kuwataka viongozi wa chama hicho kutumia fursa waliyopewa na wanachama wao, kuhakikisha kwamba wana ainisha matatizo waliyonayo walemavu wa mkoa wa Iringa na kuyafikisha katika ofisi za serikali ili yaweze kufanyiwa kazi.
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi box la mafuta hayo katibu wa Tas mkoa wa Iringa bwana Leo Sambala katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi la mafuta hayo katibu wa Mufindi bwana Andrea Kihwelo
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi mafuta hayo moja ya walemavu wa ngozi
Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi la mafuta hayo mwenyekiti wa wilaya ya Kilolo ndugu Anna Masasi .
Hivyo makala KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA
yaani makala yote KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kabati-atoa-msaada-wa-mafuta-maalum-ya.html
0 Response to "KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA"
Post a Comment