Loading...
title : KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE
link : KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE
KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi nzuri iliyofanya ya ujenzi wa jengo la makumbusho ya kisasa katika Bonde la Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu.
Kamati hiyo imesema imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambalo litawavutia watalii na wanasayansi wabobezi wa masuala ya Malikale kutembelea Makumbusho hiyo.
Kamati hiyo ilibainisha kuwa Makumbusho hiyo mbali ya kutumika kuingiza pesa kupitia watalii pia inatumika kama kielelezo na utambulisho muhimu wa taifa katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.
Hayo yalisemwa jana na Kamati hiyo wakati ilipofanya ziara ya kutembelea Ngorongoro Crater na Makumbusho ya Olduvai Gorge katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Kemilembe Luota ameipongeza Serikali pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa eneo la Olduvai Gorge linakuwa kivutio bora kwa ajili ya historia ya nchi na kivutio kikubwa cha Utalii duniani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) wakizungumza na Mbunge wa viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Zainabu Mwamwindi wakiwa wameongozana na Wajumbe Kamati hiyo wakati walipotembelea jana Jengo la Makumbusho ya Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii , Kemilembe Luota ( wa kwanza kushoto) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ‘’View Point’ kituo ambacho hutumika kuangalia bonde la Ngorongoro kabla ya kutelemka katika Bonde hilo jana wakati walipofanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Huyu ndiye Faru Fausta ni faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa katika nje ya ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuanza ziara.
Kundi la Simba wakiwa wamepumzika walipoonekana jana wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kutembelea Bonde la Ngorongoro.
Hivyo makala KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE
yaani makala yote KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kamati-ya-bunge-ya-kudumu-ya-ardhi.html
0 Response to "KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELELEA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NA MAKUMBUSHO YA OLDUVAI GORGE"
Post a Comment